Mume wake alifariki mnamo mwaka 1870 baada ya ajari mbaya ya treni ya umeme ya abiria, na kumwacha Ruete katika mazingira magumu ya kiuchumi baada ya mamlaka husika kukataa kumpatia urithi wake. Katika kupunnguza matatizo haya ya kiuchumi aliandika kitabu kinachoitwa Memoirs of an Arabian Princess from Zanzibar, kilichochapishwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani mnamo mwaka 1886, na baadaye kuchapishwa Marekani na Ireland. Kitabu hicho kilitoa historia ya mwanamke wa Kiarabu kwa mara ya kwanza. Kitabu hicho kinampa msomaji picha ya maisha ya Zanzibar kati ya mwaka 1850 hadi 1865, pamoja na picha ya ndugu zake Majid bin Said wa Zanzibar na Barghash bin Said wa Zanzibar, Masultani wa kipindi kile Zanzibar.